EBOLA-TSHISEKEDI-DRC-AFYA

Rais Tshisekedi asema maambukizi ya Ebola yatamalizika kufikia mwisho wa mwaka huu

Rais wa DRC  Félix Tshisekedi
Rais wa DRC Félix Tshisekedi Sumy Sadurni / AFP

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amesema ana matumaini makubwa kuwa, maambukizi ya Ebola, yatamalizika nchini humo kufikia mwisho wa mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi ametoa kauli hii, akiwa ziarani jijini Berlin nchini Ujerumani, baada ya kuzinduliwa kwa chanjo ya pili ya Ebola wiki hii mjini Goma.

Tangu mwezi Agosti mwaka 2018, watu zaidi ya 2,000 wamepoteza maisha na zaidi ya 3,000 kuambukizwa Ebola, Mashariki mwa nchi hiyo.

Maafisa, wanasema kuwa dozi zaidi ya 40,000 kutoka kampuni ya Johnson and Johnson, inatarajiwa kutolewa kwa wakaazi wa eneo hilo kwa awamu mbili.

Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo, maafisa wa afya wanasema kuwa watu zaidi ya 240, 000 walipata chanjo ya kwanza ya ugonjwa huu hatari.