Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Askari 24 wauawa katika shambulio kusini mwa Menaka

Askari wa Mali, Julai 2018, Bamako (Picha ya kumbukumbu).
Askari wa Mali, Julai 2018, Bamako (Picha ya kumbukumbu). © REUTERS/Luc Gnago
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Jeshi la Mali limeshambuliwa na kundi la watu wanaoshukiwa kuwa magaidi, Kaskazini mwa nchi karibu na mpaka na Niger. Shambulio lilitokea Jumatatu, Novemba 18.

Matangazo ya kibiashara

Inaonekana kuwa washambuliaji wamekuwa wamejiandalia operesheni hiyo. Watu wngi wamepoteza maisha katika shambulio hilo. Kulingana na taarifa kutoka kwa jeshi la Mali, "askari 24 na magaidi 17" wameuawa, na vifaa vingi vya adui vimeharibiwa.

"Ili kuwakabilia magaidi, wanajeshi wa Mali na Niger wanafanya operesheni ya pamoja inayoitwa" Tongo Tongo "karibu na mpaka unaozitenganisha nchi hizo mbili," imebaini taarifa rasmi. Askari wa Mali wameshambuliwa wakati wa operesheni hii.

Kulingana na vyanzo vya usalama nchini Niger, washambuliaji walikuwa kwenye gari saba na pikipiki zikiwamo pikipiki za matairi matatu, ambazo ni mali ya kituo kimoja cha afya.

Kikosi cha askari walioshambuliwa walikuwa wakienda kujiunga na vikosi vya jeshi la Niger. Hata hivyo, majeshi hayo kutoka nchi hizi mbli hayakuwa kwenye eneo moja.

Mapigano hayo yalitokea katika mji wa Ménaka. Askari wa Mali waliojeruhiwa walipokelewa nchini Niger.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.