Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-AFRIKA-WAFANYIKAZI

Wafanyakazi wagoma kuondoka katika Ofisi za Waziri Mkuu, wanataka kulipwa

Maandamano jijini Kinshasa
Maandamano jijini Kinshasa RFI/Pascal Mulegwa

Mamia ya wafanyikazi waliokuwa wanajihusisha na usafi wakati wa serikali ya rais wa zamani Joseph Kabila wameendelea kupiga kambi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga, kushikiza malipo yao.

Matangazo ya kibiashara

Wanasema kwa muda wa miezi kumi na miwili sasa, hawajalipwa mshahara wao, licha ya kuwa na mkataba wa kufanya kazi, chini ya Waziri Mkuu wa zamani Matata Mponyo.

Msemaji wa wafanyikazi hao Jean Musenge, amesema wafanyikazi hao ambao kazi yao ni kufagia barabara za jiji la Kinshasa, wanataka kulipwa pesa zao zote la sivyo wavunje mkataba uliopo.

“Tangu kuja kwa Waziri Mkuu Ilunga, hatujalipwa chochote, tunaomba tushughulikiwe au mkataba huu uvunjwe,” alisema Musenge.

Polisi wamewazingira wafanyikazi hao, ili wasiingie katika ofisi za Waziri Mkuu.

Hakuna ripoti kutoka kwa Waziri Mkuu kuhusu madai ya wafanyikazi hao.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.