Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Mwanaharakati wa haki za binadamu Almaas Elman auawa Somalia

Mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. © REUTERS/AU-UN IST Photo/Tobin Jones/Handout
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mwanaharakati maarufu wa mashirika ya kiraia Almaas Elman ameuawa kwa kupigwa risasi Jumatano, Novemba 20, wakati alikuwa akijiandaa kusafri kwa ndege kwenda mji mkuu wa Kenya, Nairobi ambako anaishi.

Matangazo ya kibiashara

Almaas Elman ameuawa wakati alikuwa akisafiri kwa gari katika eneo salama karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu ambapo wafanyakazi wengi wa mashirika ya kimataifa wanaishi.

Almaas Elman alipelekwa hospitalini mara moja, lakini alifariki dunia wakati alipokuwa akisafirishwa. Almaas Elman alikuwa mjamzito.

Binti ya mwanaharakati huyo maarufu wa amani nchini Somalia, Elman Ahmed, ambaye aliuawa mnamo mwaka 1996, alikuwa alirudi nchini Somalia kusaidia kituo kilichoanzishwa na mamake katika mipango yake ya kupambana dhidi ya unyanyasaji. Moja ya mipango ya kituo hicho ilikuwa kushawishi watoto na vijana wakubwa kuachana au kujitenga mbali na makundi yenye silaha na hivyo waweze kurudi shuleni.

Mtafiti Laetitia Bader, mtaalam wa shirika la kimatiafa la Haki za Binadamu la Human Right Watch katika ukanda wa Afrika, amesema Somalia imemkosa mtu muhimu katika maswala ya haki za binadamu.

"Familia yake imepoteza mtu muhimu, lakini pia mashirika ya haki za wanawake na haswa waathiriwa wa dhuluma ya kingono ambao ni wengi leo nchini Somalia", amesema Laetitia Bader akihojiwa na Léonard Vincent

Maafisa wa usalama wanabaini kwamba Almaas Elman ameuawa baada ya risasi hewa kumpata. "Hakuna risasi zilizofyatuliwa kwenye uwanja wa ndege au maeneo yalio karibu kabla ya tukio hilo," amesema Mohamed Omar, afisa usalama, huku akibaini kwamba Uchunguzi umeanzishwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.