AFRIKA KUSINI-UFISADI-UCHUMI

Afrika Kusini: Waziri wa zamani wa Jacob Zuma akamatwa kwa ufisadi

Bongani Bongo amekamatwa kwa kushinikiza tume ya bunge ya uchunguzi kuhusu urasimu wa shirika la serikali la umeme la Eskom (picha ya kumbukumbu).
Bongani Bongo amekamatwa kwa kushinikiza tume ya bunge ya uchunguzi kuhusu urasimu wa shirika la serikali la umeme la Eskom (picha ya kumbukumbu). © GIANLUIGI GUERCIA / AFP

Waziri wa zamani wa usalama katika utawala wa Jacob Zuma nchini Afrika Kusini, Bongani Bongo, anazuiliwa na polisi tangu Alhamisi hii, Novemba 21 kwa kashfa ya ufisadi.

Matangazo ya kibiashara

Bongani Bongo anashtumiwa kushinikiza tume ya Bunge ya uchunguzi kuhusu urasibu wa shirika la serikali la umeme la Eskom. Bongani Bongo, ambaye ni mshirika wa karibu wa rais wa zamani Jacob Zuma, atafikishwa mahakamani Januari 31. Kukamatwa kwa Bongani Bongo kumewashangaza wengi nchini Afrika Kusini.

Hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa zamani wa rais Jacob Zuma kushtakiwa kwa ufisadi. Anatuhumiwa kuwa, mwaka 2017, alijaribu kushawishi wakili wa tume ya Bunge ya uchunguzi kuhusu shirika la srikali la umeme la Eskom. Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, Bongani Bongo alimpa wakili huyo kitita cha pesa ili asiwezi kuachishwa kazi.

Waziri wa usalama wa nchi, Bongani Bongo aliteuliwa mwishoni mwa muhula wa Jacob Zuma. na mpaka sasa bado ni mbunge kutoka chama cha ANC, chama tawala. Pia anasimamia kamati ya Bunge kuhusu mambo ya ndani.

Kukamatwa kwake kunaweza kupelekea wengine wanakamatwa. Mwendesha mashtaka anayesimamia kesi za ufisadi katika serikali alisema Jumatatu kuwa ana ushahidi wa kutosha katika chunguzi mbalimbali. Ishara kwamba watu wengine wa ngazi ya juu, mawaziri na viongozi wa makampuni ya serikali, wanaweza kufikishwa mahakamani hivi karibuni. Hii ni moja ya ahadi kuu za kampeni ya Cyril Ramaphosa kwa kuonyesha kuvunjika kwa uhusiano na mtangulizi wake Jacob Zuma.