LIBYA-MAREKANI-USALAMA-SIASA

Wajumbe wa Marekani wamsihi Haftar kusitisha mashambulizi katika mji wa Tripoli

Marekani imeendelea kutoa shinikizo la kusitisha vita kwa mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya, Jenerali Khalifa Haftar, ambaye jeshi lake ANL lilizindua mashambulizi kwa lengo la kudhibiti mji wa Libya.

Mbabe aw kivita Mashariki mwa Libya Khalifa Haftar.
Mbabe aw kivita Mashariki mwa Libya Khalifa Haftar. Abdullah DOMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumapili Novemba 24, 2019 wawakilishi wa Marekani walikutana kwa mazungumzo na Jenerali Khalifa Haftar ili kujadili kuhusu uwezekano wa kusitisha mashambulizi nchini Libya, Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani imetangaza.

Ujumbe wa Marekani unaongozwa na Victoria Coates, Naibu Mshauri wa masuala ya usalama wa kitaifa katika ikulu ya White House, alikutana kwa mazungumzo na kiongozi wa kivita Mashariki mwa Libya ili kujadili kuhusu "utaratibu wa kufikia mkataba kusitisha uhasama na azimio la kisiasa kwa mgogoro wa LIbya. Wizara ya mambo ay Nje ya Maekani imesema, bila hata hivyo, kueleza sehemu mazungumzo hayo yalifanyika.

Katika taarifa yake, ameongeza kwamba wawakilishi "walibaini kwamba Marekani inaunga mkono uhuru na utulivu nchini Libya, na kuelezea wasiwasi mkubwa kufuatia mzozo huo unaochochewa na Urusi kupitia raia wa Libya.

Haftar anasaidiwa na Misri, Falme za Kiarabu na hivi karibuni mamluki kutoka Urusi, wanadiplomasia na wawakilishi wa nchi mbalimbali nchini Libya wamesema. Hata hivyo ANL inakataa kuwa haisaadiwi na nchi za kigeni katika vita vyake nchini Libya.

Wapiganaji wa kundi linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar wakiendelea na vita LIbya.
Wapiganaji wa kundi linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar wakiendelea na vita LIbya. AFP / LNA WAR INFORMATION DIVISION