Pata taarifa kuu
MOROCCO-TUNISIA-AJALI-USALAMA

Ajali mbili mbaya zaua watu 43 Tunisia na Morocco

Mabaki ya basi lililokuwa limebeba watalii kutoka Tunisia baada ya kuanguka bondeni, Desemba 1, 2019 katika mkoa wa Ain Snoussi, Kaskazini mwa Syria.
Mabaki ya basi lililokuwa limebeba watalii kutoka Tunisia baada ya kuanguka bondeni, Desemba 1, 2019 katika mkoa wa Ain Snoussi, Kaskazini mwa Syria. © AFP

Moroco na Tunisia zinaomboleza vifo vya raia wake waliofariki dunia katika ajali mbili za basi zilizotokea siku moja, Jumapili Desemba 1. Hii ni ajali mbaya kutokea katika nchi hizi mbili za Afrika Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Watu 26 wamefariki dunia nchini Tunisia, na 17 nchini Morocco.

Nchini Tunisia, basi, ambalo lilikuwa limebeba watalii kutoka nchi hiyo wenye umri ulio kati ya miaka 20 na 30, lilipoteza barabara na kuanguka bondeni. Ajali hiyo ilitokea katika Jimbo lenye milima la Ayn Snoussi, Kaskazini-Magharibi mwa Tunisia. Baada ya ajali hii iliyogharimu maisha ya watu wengi, mwendo wa kasi na ubovu wa basi vimetajwa kuwa miongoni mwa sababu kuu za ajali hiyo, ambayo ilisababisha watu 17 kujeruhiwa.

Akiulizwa na televisheni ya taifa, Waziri wa Vifaa, Nyumba na Mipango Miji, Noureddine Selmi, ambaye ametoa wito wa kusubiri kumalizika kwa uchunguzi, amebaini kwamba basi hilo lililochoka limekuwa likitumiwa kwa "miaka 20" sasa na limekuwa likiendesgwa kwa "kasi".

Mkoa wa Ain Snoussi unajulikana kwa hatari ya barabara zake, ambazo zote zina "mabango yanayoelekeza kiwango cha mwendo ambacho hautakiwa kuzidisha", amesema.

Rais mpya Kais Saied na Waziri Mkuu anayemaliza muda wake Youssef Chahed walikwenda haraka eneo la tukio jana Jumapili.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.