Pata taarifa kuu
DRC-FARDC-ADF-USALAMA

Jeshi la DRC ladai kuua waasi 80 wa ADF Beni

Desemba 3, 2014. Wilayani Beni, DR Congo. Askari wa jeshi la DRC, FARDC, na walinda amani mbele ya makao makuu ya MONUSCO, Beni.
Desemba 3, 2014. Wilayani Beni, DR Congo. Askari wa jeshi la DRC, FARDC, na walinda amani mbele ya makao makuu ya MONUSCO, Beni. MONUSCO/Abel Kavanagh
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linasema, limewauwa waasi zaidi ya 80 wa ADF Nalu Wilayani Beni, katika operesheni dhidi ya makundi ya waasi.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni operesheni inayokuja, baada ya waasi hao kuendelea kutekeleza mauaji ya raia zaidi ya 100 tangu mwezi Novemba, katika Wilaya hiyo na kuzua wasiwasi kuhusu usalama wa wakaazi wa Beni.

Wananchi Mashariki mwa nchi hiyo wameendelea kuandamana kulaani utovu wa usalama, wakishinikiza kuondoka kwa jeshi la Umoja wa Mataifa MONUSCO kwa kile wanachosema, limeshindwa kuwalinda.

Katika wii za hivi karibuni, Beni ilikumbwa na matukio mablimbali hasa, mauaji ya raia, ambapo kundi la waasi wa Uganda la ADF lilishtumiwa kuhusika na mauaji hayo ya kikatili.

Hivi karibuni Rais Felix Tshisekedi Tshilombo aliapa kuyatokomeza makundi yanayohatarisha usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwa ni pamoja na kundi hili la waasi wa Uganda la ADF.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.