Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-MAUAJI-USALAMA

Askari wa tatu na magaidi watatu wauawa kaskazini mwa Burkina Faso

Jeshi la Burkina Faso lnaendelea kukabiliana na makundi ya kigaidi, hasa kaskazini mwa nchi hiyo.
Jeshi la Burkina Faso lnaendelea kukabiliana na makundi ya kigaidi, hasa kaskazini mwa nchi hiyo. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Wanajeshi watatu wa Burkina Faso wameuawa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, wakati huu ripoti za kijeshi zikisema kuwa, magaidi 20 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi linasema, usiku wa kuamkia tarehe mbili na tatu, katika maeneo ya Toeni na Bahn, Kaskazini mwa Burkina Faso, kulitokea shambulizi lililotekelezwa na magaidi.

Katika makabiliano hayo, wanajeshi wengine saba walijeruhiwa na silaha za magaidi hao kama bastola na pikipiki zilikamatwa.

Jumapili, iliyopita, Wakirirsto 14 waliuawa baada ya kushambuliwa wakiwa katika ibada Kanisani, katika mpaka wa nchi hiyo na Nigeria.

Licha ya Burkina Faso kuwa na wanajeshi kutoka Ufaransa, pamoja na wengine kutoka nchi za Sahel kama Mali, Burkina Faso, Niger, Mauritania, Chad na wale wa Umoja wa Mataifa (MINUSMA), hali ya usalama bado ni mbaya.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.