MAREKANi-SUDANI-USHIRIKIANO

Marekani yafufua uhusiano na Sudani

Waziri Mkuu wa mpito wa Sudan, Abdallah Hamdok wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake Khartoum Agosti 21, 2019.
Waziri Mkuu wa mpito wa Sudan, Abdallah Hamdok wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake Khartoum Agosti 21, 2019. Ebrahim HAMID / AFP

Marekani imefufua uhusiano wa kushangaza na Sudani kwa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa mpito Abdallah Hamdok, anaendelea na ziara nchini humo kuomba vikwazo dhidi ya nchi yake visitishwe kwa 'kuunga mkono ugaidi.'

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya Waziri Mkuu wa mpito wa Sudani nchini Marekani ni ziara ya kihistoria.

"Marekani na Sudani zimeamua kuanza mchakato wa kubadilishana mabalozi baada ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa muda wa miaka 23," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amesema. Hivi karibuni balozi wa Marekani ateteuliwa huko Khartoum.

"Uamuzi huu ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili, Sudani na Marekani, haswa wakati huu ambapo serikali ya mpito inayoongozwa na raia inafanya mageuzi makubwa," Mike Pompeo ameongeza katika taarifa yake.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulikuwa umedorora kabisa kwa kipindi cha miaka 30 ya utawala wa Omar al-Bashir, aliyepinduliwa madarakani kufuatia maandamano makubwa.

Tangu mwaka 1993, wakati Rais Bashir alimpokea kiongozi wa mtandao wa al-Qaeda Osama bin Laden, Sudan iliwekwa kwenye orodha nyeusi ya "mataifa yanayounga mkono ugaidi".

Mwaka 1998, baada ya mashambulizi makubwa ya Al-Qaeda dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania, Washington iliendesha mashambuizi ya anga nchini Sudani.

Tangazo la kufufua uhusiano kati ya Sudani na Marekani linakuja wakati Waziri Mkuu wa mpito anaendelea na ziara yake Washington.

- Hii ni ziara ya kihistoria -

Ni mara ya kwanza tangu mwaka 1985 kiongozi wa Sudan kupokelewa na maafisa wa serikali ya Marekani katika mji mkuu wa Marekani.

Jumanne wiki hii, Abdallah Hamdok alikutana kwa mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin, ambaye "alikaribisha" nia yake ya mageuzi na akasisitiza kuhusu vita dhidi ya utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi.