MAURITANI-WAHAMIAJI-AJALI

Wahamiaji wengi wafariki dunia katika pwani ya Mauritania

Abiria 83 walifanikiwa kuogelea hadi nchi kavui baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Mauritania Desemba 4, 2019. (picha ya kumukumbu)
Abiria 83 walifanikiwa kuogelea hadi nchi kavui baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Mauritania Desemba 4, 2019. (picha ya kumukumbu) © REUTERS/Mauro Buccarello

Wahamiaji zaidi ya hamsini na nane wamekufa maji baada ya boti waliokuemo kuzama katika pwani ya Mauritania. Walikuwa 150 wakitokea Gambia katika boti kabla ya boti hiyo kuzama Jumatano jioni wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Miili hamsini na nane imepatikana wakati huu na wahamiaji 85 wameokolewa. Kulingana na manusura, boti hiyo iliondoka Gambia Novemba 27 ikielekea Uhispania.

Njia hii iliyotumiwa iliwahi kutumiwa katika siku za nyuma, na hivi wahamiaji wameanza sasa kuitumia. Yote hayo huenda ni kutokana na usalama kuimarika katika bahari ya Mediterranian. Wanaosafirisha wahamiaji hao hufanya waachotaka ili mradi tu wapate fedha.Wanajaribu kutumia njia yoyote ile kwa kuwasafirisha wahamiaji wanaotaka kiuingia Ulaya.

"Wengi wao walikuwa wahamiaji haramu ambao walikuwa awmeharibu kusafiri hadi nchini Uhispania wakitokea Gambia," Wizara ya Mambo ya Ndani ya Mauritania imebaini katika taarifa.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) imesema abiria 83 wameweza kuogelea hadi nchi kavu. "Mamlaka ya Mauritania inashirikiana vyema na ofisi zetu zilizopo Nouadhibou," amesema Laura Lungarotti, mkuu wa ujumbe wa IOM nchini Mauritania.

"Kipaumbele chetu ni kuwahudumia manusura na kuwapa msaada unaohitajika," ameongeza.

Waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya Nouadhibou.