Pata taarifa kuu
DRC-BENI-ADF NALU-MAUAJI

Mashirika ya kiraia yataka ICC kuchunguza mauaji yanayoendelea kutokea Wilayani Beni

Kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya ICC Fatou Bansouda
Kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya ICC Fatou Bansouda icc-cpi.int
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mashirika ya kiraia nchini DRC na kwingineko duniani, yanataka Ofisi ya mwendesha Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, kuchunguza mauaji yanayoendelea Wilayani Beni Mashariki mwa nchi hiyo na wahusika wote kufunguliwa mashtaka.

Matangazo ya kibiashara

Wito huu umetolewa wakati mkutano wa nchi wanachama wa Mahakama ya ICC uliofanyika mjini Hague nchini Uholanzi.

Mashirika ya kiraia nchini DRC yakiongozwa na Joseph Dunia Ruyenzi yanataka ofisi ya kiongozi wa mashtaka kuanza mara moja uchunguzi huko Beni.

Tangu mwezi Novemba watu zaiid ya 100 wamepoteza maisha Wilayani Beni, baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wanaoaminiwa kuwa waasi wa ADF Nalu.

Kutokana na utovu wa usalama, jeshi la serikali na lile la kulinda amani MONUSCO limetangaza operesheni ya pamoja dhidi ya makundi ya waasi Mashariki mwa nchi hiyo.

Licha ya operesheni hii, mauaji yameendelea kuripotiwa kila wiki wilayani Beni, huku watu wakiishi kwa hofu na hata kushindwa kwenda kazini.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.