Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-ITURI-EBOLA-MSF

Shirika la MSF laondoa wafanyikazi wake mkoani Ituri

Mapambano dhidi ya Ebola Mashariki mwa DRC
Mapambano dhidi ya Ebola Mashariki mwa DRC REUTERS/James Akena
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Shirika la kimataifa la madaktari wasiokuwa  na mipaka MSF limetangaza kusitisha shughuli zake kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika  mkoa wa Ituri kutokana na kile ilichosema ni mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi dhidi ya wafanyakazi wake walioko mstari wa mbele kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya kifo cha mwandishi wa Habari mapema mwezi Novemba katika eneo la Lwemba.

Ive Ndjadi afisa wa juu wa MSF, amesema vitisho dhidi ya wafanyikazi hao wa afya lakini pia kuharibiwa kwa miundo mbinu muhimu ya kusaidia katika mapambano hayo, imeharibiwa.

“Kulikuwa na jaribio la kuingia ndani ya kituo cha afya cha Biakato Mine, na hatukuwafahamu kwa hivyo tukaamua kuhamisha shughuli zetu, “ alisema Ndjadi.

Mashirika ya kiraia yanahofia kuwa, kuondoka kwa maafisa wa MSF kunaweza kusababisha maambukizi zaidi, wakati huu Professa Jean-Jacques Muyembe anayeongoza kamati ya kupambana na maambukizi ya Ebola, akitoa wito kwa wakaazi wa eneo hilo kuendelea kushirikiana kutokomeza ugonjwa huu.

“Tunawaomba wananchi kuwa na mtazamo na tabia sawa kama watu wa Beni na Butembo na maeneo mengine ambayo maambukizi haya yamedhibitiwa, la sivyo mambo yatakuwa mabaya zaidi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.