DUNIA-HAKI ZA BINADAMU

Dunia yaadhimisha siku ya kimataifa ya Haki za Binadamu

Tarehe 10 Desemba 1948 ilitangazwa Azimio na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu Tamko la Haki za Binadamu na tangu mwaka 1950 kuanza rasmi kufanyika Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.
Tarehe 10 Desemba 1948 ilitangazwa Azimio na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu Tamko la Haki za Binadamu na tangu mwaka 1950 kuanza rasmi kufanyika Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Khananastasia (Getty Images)

Dunia hivi leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya Haki za Binadamu, huku ofisi ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa ikieleza kuguswa na kuendelea kuongezeka kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye mataifa mengi.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo tofauti na maadhimisho ya miaka mingine, mwaka huu maadhimisho haya yanafanyika, huku vijana wakitakiwa kuwa mstari wa mbele na kusimama kidete kutetea haki za binadamu.

Kiini cha Siku hiyo ni kuelimisha na kuhamasisha watu kulingana na binadamu alivyo na kukumbusha hatua zilizopigwa na jamii katika kutekeleza sula la heshima ya binadamu wote, dhidi ya utumwa na kukandamizwa kwa haki binafsi

Tarehe 10 Desemba 1948 ilitangazwa Azimio na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu Tamko la Haki za Binadamu na tangu mwaka 1950 kuanza rasmi kufanyika Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Tamko hili lina Ibara 30, ambapo ibara ya kwanza ni “Watu wote wamezaliwa huru hadhi na haki zao ni sawa wote wana akili na wana dhamiri.

Leo ni siku ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni tarehe ya kukumbuka ya kupitishwa kwa azimio la haki za binadamu duniani. Shirika la Haki za Binadamu (LHRC) la Umoja wa Mataifa kwa maana hiyo linatimiza miaka 70. Azimio hilo lilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kunako tarehe 10 mwezi Desemba mwaka 1948 huko Paris mji mkuu wa Ufaransa.

Kutokana na hili lilipatiwa jina la tamko la haki za binadamu na na wakati huo huo hati hiyo ikaweka viwango vya pamoja vya haki za binadamu kwa wote na mataifa yote.

Azimio hilo, kwa mara ya kwanza liliweka misingi ya haki za binadamu inayokubalika kimataifa na inayopaswa kulindwa popote pale duniani. Hadi sasa Azimio hilo limetafsiriwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo hata Kiswahili.