ETHIOPIAiABIY-TUZO YA AMANI YA NOBEL

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mshindi wa 10 wa Tuzo ya Amani ya Nobel Afrika

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. AFP/Monirul BHUIYAN

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amepokea rasmi tuzo ya Amani ya Nobel mjini Oslo, ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kuutatua mzozo wa mpaka na nchi jirani Eritrea.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wanaharakati wa kimataifa pamoja na wadau wengine wakiwemo baadhi ya wanachama wa Kamati ya Nobel ya Norway wametilia shaka kuona tuzo hiyo haitasaidia wala haisadii kwa vyovyote upatikanaji wa mshikamano wa kitaifa kufuatia mgogoro wa kisiasa uanaoshuhudiwa ndani ya nchi hiyo.

Tuzo hiyo imelenga pia kutambua juhudi za Waziri Abiy mwenye umri wa myaka 43, kuleta amani na maelewano nchini Ethiopia na katika kanda yote ya Kaskazini Mashariki mwa Afrika.

Akielezea sababu za kuchaguliwa waziri mkuu huyo, mwenyekiti wa kamati ya Nobel Bi Berit Reiss-Andersen amesema "Kamati ya Nobel ya Norway imeamua kumtunukia tuzo ya amani ya Nobel, waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali kwa juhudi zake za kusaka amani na ushirikiano wa kimataifa na hasa kuupatia ufumbuzi mzozo wa mpakani pamoja na nchi jirani ya Eritrea."

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ndiye mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel - mshindi wa kumi barani Afrika. Ametunukiwa kwa juhudi zake za upatanisho. Tuzo ya kwanza ya Amani ya Nobel ilienda Afrika mnamo 1960.

Albert Luthuli alikuwa Mwafrika wa kwanza kupokea Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 1960 kwa sera yake ya amani dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Harakati za ukombozi zilizuiliwa na serikali ya kibaguzi, kumpiga marufuku Luthuli. Hakuweza kupokea tuzo hiyo hadi mwaka mmoja baadaye, marufuku ya kusafiri ikaondolewa kwa siku kumi, Luthuli alisafiri kwenda Oslo kupokea tuzo yake.