Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-UCHAGUZI

Uchaguzi wasusiwa na idadi kubwa ya raia Algeria

Zoezi la kupiga kura katika kituo cha kupigi kura Algiers, katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Algeria, Desemba 12, 2019.
Zoezi la kupiga kura katika kituo cha kupigi kura Algiers, katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Algeria, Desemba 12, 2019. REUTERS/Ramzi Boudina
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mamlaka inayosimamia uchaguzi nchini Algeria imetangaza usiku wa kuamkia leo Ujumaa kwamba wapiga kura 39.93 wamepiga kura katika uchaguzi huu wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo zoezi hilo liligubikwa na maandamano ya raia kwenye mji mkuu Algiers na kuvamiwa kwa vituo vya kupigia kura.

Kiwango cha ushiriki kilikuwa cha chini, na hivyo kuweka mashakani mamlaka.

Kiwango hiki cha ushiriki kilikuwa kinatarajiwa. Mamlaka inayosimamia uchaguzi ilitangaza kiwango hicho baada ya usiku wa manane wakati wagombea wanne kati ya watano wakijitangazia ushindi wao huku wakibaini kwamba wako tayari kushiriki katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais. Kauli hizo tofauti zimeendelea kuzua sintofahamu nchini Algeria.

Mamlaka ya kusimamia uchaguzi hatimaye ilitangaza kwamba watu waliopiga kura walifikia asiliamia 39.93 ikilinganishwa na idadi ya wapiga kura waliojiorodhesha. kiwango hicho kiko chini alama kumi ikilinganishwa na mwaka 2014. Ni kiwango cha chini kabisa cha ushiriki katika uchaguzi wa urais nchini Algeria. Jumla wapiga kura 9.6 milioni ndio walipiga kura, kati ya wapiga kura milioni 43 waliorodheshwa.

Takwimu zinaonesha kuwa raia 6 kati ya 10 nchini Algeria hawakushiriki zoezi la upigaji kura, hali inayoashiria kuwa mamilioni ya raia walikuwa wanapinga kufanyika kwa uchaguzi huo.

Raia wanataka kwanza kuondolewa kwa wagombea na viongozi waliokuwa chini ya utawala wa rais Abdelazizi Bouteflika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.