COTE D'IVOIRE-SORO-SIASA-USALAMA

Ndege iliyokuwa ikimbeba Guillaume Soro yalazimika kutua Ghana

Vikosi vya usalama vya Côte d'Ivoire vikizingira makaazi ya spika wa zamani wa Bunge Guillaume Soro, Abidjan, Côte d'Ivoire, Desemba 23, 2019.
Vikosi vya usalama vya Côte d'Ivoire vikizingira makaazi ya spika wa zamani wa Bunge Guillaume Soro, Abidjan, Côte d'Ivoire, Desemba 23, 2019. © Edouard Dropsy / RFI

Kiongozi wa zamani wa waasi nchini Côte d'Ivoire na mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2020 Guillaume Soro, ambaye alikuwa katika ndege binafsi akisafiriki kuelekea Abidjan, hatimaye ameamua kutua Accra, nchi jirani ya Ghana. Guillaume Soro anasakwa na waranti uliotolewa na Côte d'Ivoire.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Côte d'Ivoire imepiga marufu Guillaume Soro kurudi nchini humo. Spika wa zamani wa Bunge la taifa na mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2020 alitarajiwa kuwasili mapema Jumatatu alaasiri jijini Abidjan baada ya kutokuwepo nchini humo kwa zaidi ya miezi sita. Siku ya Ijumaa, mambo yote yalikuwa yamekamilika ili Guillaume Soro aweze kurudi nchini Côte d'Ivoire. Idhini kupita kwenye anga ya Abidjan na kutua katika jiji hilo ilikuwa imetolewa na uongozi wa jeshi la anga na majini. Kwa ziara rasmi ya rais wa Ufaransa mwisoni mwa wiki iliyopita nchini Côte d'Ivoire, wengi walikuwa na matumaini kwamba spika wa zamani wa Bunge la taifa nchini humo atarudi kuanza kampeni yake kwa uchaguzi wa urais wa mwaka 2020. Hata hivyo aliweza kusitisha safari yake ya kurudi Abidjan siku ya Jumapili kama ilivyokuwa ilipangwa awali na kuahirisha hadi jana Jumatatu.

Jana Jumatatu mamlaka chini Côte d'Ivoire ilipiga marufuku mtu yeyote kukaribia makaazi ya Guillaume Soro. Hata kaka yake hakuweza kukanyaga kwenye makaazi yake.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na serikali, Guillaume Soro anashtumiwa " makosa ya utakatishaji fedha, kutaka kuhatarisha usalama wa taifa na kupitisha mlango wa nyuma mabilioni ya fedha, " zinazokadiriwa kufikia faranga za CFA biloni 1.5.