NIGER-USALAMA

Askari kumi na wanne wauawa katika shambulio Tillaberi

Wanajeshi wa Nigeria wakipiga doria (picha ya kumbukumbu).
Wanajeshi wa Nigeria wakipiga doria (picha ya kumbukumbu). © ISSOUF SANOGO / AFP

Niger inaomboleza tena vifo vya askari wake kumi na wanne walio uawa katika shambulio jipya lililotokea Jumatano wiki hii katika Jimbo la Tillaberi, Magharibi mwa nchi. Kwa mujibu wa mamlaka nchini humo, askari 14 waliuawa katika shambulio la "magaidi wenye silaha za kivita".

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) walikuwa wakirudi baada ya kumaliza zoezi la kujiandikisha walilokuwa wakisimamia katika vijiji mbali mbali kwa kujiandalia Uchaguzi Mkuu ujao. Wakati huo huo 'magaidi wenye silaha za kivita' waliendesha shambulio la kuvizia dhidi ya askari walio kuwa wakisindikiza msafara wa magari ya maafisa hao wa tume ya uchaguzi, kulingana na taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani.

Kwa mujibu wa mamlaka nchini Nigeria, 'kulikuwa na mapigano makali'. Katika mapigano hayo polisi saba na askari saba wa kikosi cha ulinzi wa taifa walipoteza maisha. Askari mmoja wa kikosi cha ulinzi wa taida hajulikani aliko. Washambuliaji wengi waliuawa, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema, bila hata hivyo kuelezea idadi halisi ya waathiriwa.

Ikiwa maafisa wa tume ya uchaguzi (CENI) hawakupata hasara yoyote katika shambulio hilo lililotokea katika eneo la Sanam, hali hiyo inaonesha kuwa bado kuna tatizo kubwa: "hali hii inaonyesha matatizo ambayo viongozi wa tawaa wa eneo hilo wanakumbana nalo kuandaa uchaguzi wa mwaka 2020", amebaini mmoja wa waangalizi, huku akihoji ikiwa tume huru ya uchaguzi itaweza kuandika wapiga kura wote kwa nchi nzima.