COTE D'IVOIRE-SORO-SIASA-USALAMA

Mashitaka dhidi ya Guillaume Soro yawekwa wazi

Guillaume Soro, katika kikao cha Bunge, Februari 8, 2019, Cote d'Ivoire.
Guillaume Soro, katika kikao cha Bunge, Februari 8, 2019, Cote d'Ivoire. REUTERS/Thierry Gouegnon/File Photo

Ofisi ya Mashitaka nchini Cote d'Ivoire imeweka wazi mashtaka yanayomkabili spika wa zamani wa bunge la nchi hiyo Guillaume Soro. Kulingana na taarifa iliyotolewa na ofisi ya mashitaka, Guillaume soro 'alikuwa akiandaa uasi wa kiraia na wa kijeshi' ili 'kuchukuwa madaraka'.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka, mashtaka haya yanahusiana haswa na sauti iliyorekodi ambayo iliyotolewa na idara ya ujasusi ya cote d'Ivoire.

Richard Adou amedai kuwa silaha pia ziligunduliwa wakati wa msako. Msako ambao hakutaja ulifanyika lini na katika eneo gani.

Mwendesha mashtaka wa jamhuri Adou Richard ameonyesha 'ushahidi' ambao amesema anao dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa waasi na wapiganaji wake kufuatia msako huo na vitu vilivyo kamatwa.