Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Guinea-Bissau: Matokeo ya uchaguzi kutangazwa Jumatano

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Guinea Bissau.
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Guinea Bissau. © C. Idrac/RFI
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Wananchi wa Guinea-Bissau wanaenelea kusubiri kutangazwa kwa rais mpya baada ya kupiga kura Jumapili Desemba 29. Wengi wanatarajia kufunua ukurasa mpya kufuatia mdororo wa usalama unaoendelea kuikumba nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Matangazo ya kibiashara

Raia wa Guinea wanatarajia kuwa uchauzi huo wa urais utaleta suluhisho la mgogoro wa kisiasa uliodumu miezi kadhaa nchini humo.

Tayari mmoja wa wagombea ametoa malalamiko yake akibaini kwamba uchaguzi huo wa duru ya pili umegubikwa na udanganyifu mkubwa. Zoez a kuhesabu kura limeanza mara baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa, saa 5:00 jioni.

Wapiga kura 700,000 na jamii ya kimataifa wana imani kwamba uchaguzi huo utapelekea kuondoa hali ya sintofahamu iliyojitokea kati ya wasiasa ambao wamekuwa wakishtumiwa makosa ya rushwa na kushindwa kukidhi mahitaji ya msingi ya raia ambao ni miongoni mwa masikini zaidi ulimwenguni.

Jumapili jioni, msemaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CNE), Felisberta Vaz Moura, alisema kuwa matokeo ya uchaguzi yatatangazwa Jumatano, Januari 1. Aliwataka 'wagombea na vyombo vya habari vya kitaifa na vile vya kigeni kujizuia kutoa taarifa yoyote inayohusiana na matokeo ya uchaguzi'.

Watu wapatao 700,000 wenye haki ya kupiga kura, wamepiga kura kumchagua rais mpya kati ya wagombea wawili waliowahi kuwa mawaziri wakuu wa nchi hiyo. Domingos Simoes Pereira, kutoka chama tawala cha PAIGC, na Umaro Sissoco Embalye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Guinea-Bissau. Rais aliye madarakani Jose Mario Vaz alitolewa katika kinyang'anyiro hicho wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi mnamo mwezi Novemba.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.