SOMALIA-MAREKANI-USALAMA

Marekani yafanya shambulizi dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab

Uharibifu unaoendelea kutekelezwa na Al Shabab Somalia.
Uharibifu unaoendelea kutekelezwa na Al Shabab Somalia. REUTERS/Feisal Omar

Marekani imesema jeshi lake barani Afrika, US Africa Command, AFRICOM, limewauwa magaidi wanne baada ya kutekeleza shambulizi la angaa dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab nchini Somalia.

Matangazo ya kibiashara

Hili ni shambulizi ambalo limekuja, baada ya kutokea kwa shambulizi mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Mogadishu na kusababisha vifo vya watu 79.

Jeshi la Marekani nchini humo linasema mashambulizi hayo mawili, yaliwalenga magaidi ambao wanaendelea kuwauwa raia wasiokuwa na hatia, na yalilenga magari ya kundi hilo katika eneo la Qunyo Barrow na Caliyoow Barrow.

Somalia inaendelea kukumbwa na mashambulizi ya kundi la Al Shabab, ambayo yamegharimu maisha ya watu wengi na watoto wengi amekuwa ni mayatima kutokana wazazi wengi aliuawa katika mashambulizi hayo.