COTE D'IVOIRE-BLE GOUDE-HAKI

Charles Blé Goudé: Ninamuomba rais Ouattara atukutishe pamoja

Charles Blé Goudé mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Januari 28, 2016.
Charles Blé Goudé mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Januari 28, 2016. Peter Dejong / POOL / AFP

Waziri wa zamani wa Laurent Gbagbo na kiongozi wa zamani vuguvugu la vijana wa chama tawala katika utawala wa Laurent Gbagbo, amemuomba rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara kuwakutanisha pamoja.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja siku chache baada ya mahakama ya Abidjan kumhukumu Charles Blé Goudé kifungo cha miaka ishirini kwa makosa ya mauaji, ubakaji na mateso, hukumu aliyopewa akiwa nje ya nchi hiyo.

Kabla ya hukumu hii Ble Goude ambaye alikuwa mshirika wa karibu rais wa zamani Laurent Gbagbo na kiongozi wa vijana katika chama tawala wakati huo nchini Cote d'Ivoire, alikuwa ameondolewa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC.

Licha ya uamuzi huo wa ICC, serikali ya Cote d'Ivoire ilimfungulia mashtaka mapya dhidi yake, kwa madai ya kutekeleza tuhuma hizo wakati wa mzozo wa kisiasa kati ya mwaka 2010-2011.

Mwanasiasa huyo licha ya kuondolewa mashtaka, bado yupo nchini Uholanzi wakati huu ofisi ya kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya ICC ikitarajiwa kukataa rufaa.

Machafuko ya kisiasa nchini Cote d'Ivoire yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000.