LIBYA-EU-UTURUKI-USALAMA

Umoja wa Ulaya watahadharisha kuhusu hali nchini Libya

Mapigano yaendelea kupamba moto Libya.
Mapigano yaendelea kupamba moto Libya. REUTERS/Ismail Zitouny

Siku moja baada ya rais wa Uturuki kutangaza kwamba zoezi la kuwatuma askari wa nchi hiyo nchini Libya limeanza, Umoja wa Ulaya umetoa tahadhari kuhusu hali ya mvutano inayoendelea nchini Libya.

Matangazo ya kibiashara

Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Josep Borell ameonya kwamba huenda kukashuhudiwa mapigano makali zaidi katika mji mkuu wa Libya Tripoli, akitoa wito wa suluhisho la mzozo huo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga kukutana leo Jumatatu kujadili hali ya Libya, baada ya kauli hiyo ya rais Recep Tayipp Erdogan.

Hata hivyo Rais wa Uturuki amesema Uturuki iko tayari kusaidia serikali ya umoja wa kitaifa yenye makao yake makuu mjini Tripoli. Serikali hiyo ndio serikali halali inayotambuliwa na jamii ya kimataifa. Hata hivyo baadhi ya nchi za kiarabu ikiwa ni pamoja na Misri zinamuunga mkono mbabe wa kivita, Mashariki mwa Libya, Marshal Khalifa Haftar.

Hivi Karibuni Misri ilionya Uturuki kutuma askari wake nchini Libya, ikibaini kwamba itakuwa ni moja ya uchochezi wa vita nchini humo.

Kulingana na Wizara ya Afya mjini Tripoli, watu thelathini walifariki dunia Jumamosi baada ya shambulizi la roketi katika shule inayotoa mafunzo ya kijeshi mjini Tripoli,