MALI-USALAMA

Wanajeshi watano wa Mali wauawa katika mlipuko Alatona

Jeshi la Mali likipiga doria huko Anderamboukane, katika mkoa wa Menaka, Machi 22, 2019.
Jeshi la Mali likipiga doria huko Anderamboukane, katika mkoa wa Menaka, Machi 22, 2019. Agnes COUDURIER / AFP

Askari wanato wa Mali wameuawa katika mlipuko wa bomu lililotengenezwa kienyeji katikati mwa nchi, Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali amebaini.

Matangazo ya kibiashara

"Ujumbe wa kikosi cha jeshi la Mali (FAMA) umekumbwa na shambulio la kushtukiza la bomu lililotengenezwa kienyeji mapema leo asubuhi.

Mpaka sasa askari watano ndio inasadikiwa kuwa wameuawa katika mlipuko huo, huku magari manne yakiharibika vibaya," Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali ya Mali Yaya Sangare ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Idadai ya jeshi imeongezwa ili kukabiliana na maadui," ameongeza.

Tukio hilo limetokea katika Alatona, mji uliopo kati ya Ségou na mpaka wa Mauritania, kwa mujibu wa waziri wa Mawasiliano. Eneo nzima la Sahel - haswa Mali, Niger na Burkina Faso - sasa ndio zinalengwa na mashambulizi mabaya zaidi yanayotekelezwa na makundi kadhaa ya wapiganaji wa Kiislamu, licha ya kuepo kwa vikosi vya kikanda, askari 4,500 wa jeshi la Ufaransa linalopambana dhidi ya ugaidi (Barkhane) na jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Mali.

Wanamgambo wa Kiislamu wameua zaidi ya wanajeshi 140 wa Mali kati ya mwezi Septemba na Desemba, kwa mashambulizi ambayo yamekuwa yakiendelea tangu mwaka 2013.