Pata taarifa kuu
DRC-UBELGIJI-USHIRIKIANO

DRC: Ofisi kuu ya balozi ndogo za Ubelgiji kufunguliwa Lubumbashi

Katikati mwa mji wa Lubumbashi (picha ya kumbukumbu).
Katikati mwa mji wa Lubumbashi (picha ya kumbukumbu). © Wikimedia Commons CC BY-SA 2.5 Oasisk

Ofisi kuu ya balozi ndogo za Ubelgiji jijini Lubumbashi itafunguliwa upya leo Jumatatu Januari 13 baada ya kufungwa kwa kipindi cha miaka miwili. Huu ni mwendelezo wa kuweka sawa uhusiano kati ya Kinshasa na Brussels, hali ambayo imewezeshwa na mabadiliko ya utawala nchini DRC tangu mwezi Januari 2019.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi kuu ya balozi ndogo za Ubelgiji jijini Lubumbashi ina mamlaka makubwa katika mkoa mzima wa zamani wa Katanga.

Kurejeshwa kwa uhusiano huu kati ya nchini hizi mbili ulipitishwa wakati wa ziara ya rais wa DRC Félix-Antoine Tshisekedi katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels. Pande zote mbili zilikubaliana kufungua tena ofisi kuu ya balozi za Ubelgiji jijini Lubumbashi na ile ya DRC huko Anvers.

Uhusiano kati yaDRC na ubelgiji ulikuwa ulidorora mara kadha kwa miaka mingi tangu utawala wa Marshal Mobutu, na haswa katika miaka ya mwisho ya utawala wa Kabila.

Ubelgiji ilionekana adui wa DRC, baada tu ya kuweka wazi msimamo wake, kwa kuitaka serikali iliyokuepo wakati wa utawala wa Joseph Kabila kuheshimu Katiba ya nchi na kumuomba rais Kabila kutoendelea kusalia madarakani.

Tangu alipoingia madarakani, Felix Tshisekedi, ameendelea kufanya juhudi za kurejesha uhusiano kati ya DRC na Ubelgiji katika nyanja mbalimbali.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.