Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA-USALAMA-HAKI

Sudan: Mahakama yatoa waranti dhidi ya ndugu wawili wa Omar al-Bashir

L'ex-président soudanais Omar el-Béchir, ici le 5 avril 2019 à Khartoum.
L'ex-président soudanais Omar el-Béchir, ici le 5 avril 2019 à Khartoum. © REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Mahakama nchini Sudan imetoa waranti dhidi ya kaka wawili wa Rais wa zamani wa Omar al-Bashir. Wanatuhumiwa makosa ya ufisadi na kujitajirisha kinyume cha sheria.

Matangazo ya kibiashara

Watu hao ni Ali el-Béchir na Mohamed el-Béchir. Wote wawili wanatuhumiwa kumiliki ardhi iliyopatikana kwa njia ya utapeli jijini Khartoum ambayo rais wa zamani Omar al-Bashir alijenga kituo kikuu cha kidini.

Lakini mbali na tuhuma hizo, familia ya Omar al-Bashir inashutumiwa kutumia uhusiano wake na rais huyo wa zamani kwa kujitajirisha kinyume cha sheria.

Karibu familia nzima ya Omar al-Bashir inasakwa na mahakama na baadhi wamesha wekwa kizuizini.

Ndugu wanne wa dikteta huyo wa zamani, wote wanatuhumiwa makosa ya ufisadi.

Kaka mkubwa katika familia ya al-BAshir, Abdallah Hassan al-Bashir, ambaye ni daktari, alikamatwa saa 24 tu baada ya Omar el-Bashir kukamatwa. Abdallah Hassan al-Bashir anaongoza zaidi katika familia hiyo kwa ufisadi, kwa mujibu wa mwanasheria Mahmoud al-Sheik.

"Hapo awali alikuwa daktari, lakini mapema mnamo mwaka 1990, mdogo yake alipoingia madarakani, alianza kununua kampuni katika nyanja zote. Ana idadi isiyohesabika ya makampuni, lakini zaidi ya yote alikuwa anauza pasi za kusafiria za Sudan kwa raia wa Syria. Alikuwa akipokea dola 10,000 kwa pasipoti moja, " Mahmoud al-Sheik amebaini.

Ndugu wengine wawili wa Omar al-Bashir, Abbas al-Bashir na Ali al-Beshir, walikimbilia Uturuki wiki moja tu baada ya Omar al-Bashiri kukamatwa.Wanashutumiwa kuwa walitumia ushawishi wao kwa kaka yao kwa kupata mikataba, kuanzisha makampuni na kutolipa ushuru, walikuwa na zaidi ya makampuni ishirini kwenye madini, petroli, ujenzi, kuagiza na kuuza nje ya nchi.

Ndugu wa nne wa Omar al-Bashir, Mohammed al-Bashir, anayesakwa na mahakama nchini Sudan, ni daktari nchini Uingereza. Na mke wa pili wa Omar al-Bashir, Widad Babiker - aliyekamatwa mwezi uliopita - anatuhumiwa kumiliki pesa kinyume cha sheria na kupata ardhi kwa njia ya utapeli.

Kwa mujibu wa mwanasheria anayeshughulikia masuala ya ufisadi, Mahmoud al-Sheik, anakadiria kuwa mali za familia ya Al-Bashir zina thamani ya dola bilioni kadhaa za Markani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.