Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFRIKA-MASHARIKI YA KATI-USALAMA

Washington yataka kupunguza vikosi vyake barani Afrika na Mashariki ya Kati

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Jenerali Mark Milley, Washington, Januari 8, 2020.
Waziri wa ulinzi wa Marekani, Jenerali Mark Milley, Washington, Januari 8, 2020. © REUTERS/Tom Brenner

Marekani inataka kupunguza idadi ya wanajeshi wake barani Afrika. Afisa wa juu wa Marekani Jenerali Mark Milley, amesema hilo linaweza kutokea au wanajeshi hao kuhamishwa katika maeneo mengine ya dunia.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi Mark Esper, hata hivyo hajafanya uamuzi huo,ili kufahamu ni hatua gani zitachukuliwa. Rais Trump amekuwa akitaka jeshi la muungano wa NATO, kuchukua jukumu la kupambana na ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo Wakuu wa nchi tano za Ukanda aw Sahela waliokuwa wakishiriki mktano na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wamebaini kwamba "wanathamini msaada muhimu wa Marekani" na wana matumaini kwamba msaada huu utaendelea.

Jenerali Mark Milley yuko Brussels kuanzia Jumanne hii na kesho Jumatano kwa mkutano wa kamati ya jeshi la NATO pamoja na wenzake.

Jenerali Mark Milley amethibitisha kuwa vikosi vya Marekani vitapunguzwa Barani Arika na MAshariki ya Kati na kuhamishwakatika Ukanda wa Pacific.

"Vikoi vya Marekani barani Arika na Mashariki ya Kati vitapunguzwa kisha kuhamishwa au kutumwa katika Ukanda wa Pacific.

Jeshi la Marekani barani Afrika, AFRICOM, lilianzishwa mnamo mwaka 2007. Makao yake makuu yapo Ujerumani, lakini wanajeshi elfu saba wanapiga kambi barani Afrika, nusu yao wakiwa katika mji wa Djibouti. Askari wengine 2000 wamepelekwa kwenye ujumbe wa mafunzo kwa maslahi ya majeshi ya kitaifa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.