Pata taarifa kuu
DRC-AJALI-USALAMA

Kumi na tano waangamia baada ya boti lao kuzama katika Ziwa Mai-Ndombe

Ziwa Mai-Ndombe , DRC, ambapo watu 15 walikufa maji baada ya boti kuzama.
Ziwa Mai-Ndombe , DRC, ambapo watu 15 walikufa maji baada ya boti kuzama. Wikimédia/J. Claeys Boùùaert

Watu 15 wamepoteza maisha na wengine hawajulikana walipo, baada ya kuzama kwa boti katika Ziwa Mai-Ndombe, Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Meya wa mji wa Inongo amesema huenda idadi ya watu waliopoteza maisha ikaongezeka, baada ya ajali hiyo kutokea siku ya Jumatatu, wakati huu, juhudi zikiendelea kutafuta miiili zaidi.

Ripoti zinasema kuwa boti hiyo ilikuwa inawasafisha watu 30 waliokuwa wametokea msibani, Kilomita 35 kutoka eneo la ajali hiyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, ajali kama hizi zimeendelea kushuhudiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nchi ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya miundombinu na watu wengi hutumia usafiri wa majini, kutokana na ukosefu wa barabara inayoweza kuunganisha maeneo mbalimbali.

Watalaam wanasema kuwa, ajali hizi zimeendelea kuongezeka kwa sababu, boti hizo ambazo hazifanyiwi ukarabati mara kwa mara na kuwasafirisha abiria kupita kiasi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.