DRC-USALAMA-FARDC-WAASI

Wanajeshi wawili wa FARDC wauawa wilayani Rutshuru mashariki mwa DRC

Wapiganaji waasi waFDLR wakiwa wamekusanywa katika kambi mjini Kisangani, DRC, mbele ya mjumbe wa katibu mkuu wa UN David Gressly, July 2015.
Wapiganaji waasi waFDLR wakiwa wamekusanywa katika kambi mjini Kisangani, DRC, mbele ya mjumbe wa katibu mkuu wa UN David Gressly, July 2015. MONUSCO/Abel Kavanaugh

Wanajeshi wawili wa serikali ya DRC wameuawa na kambi yao kuchomwa moto baada ya kushambuliwa na waasi waFDLR Rudi katika eneo la Kakondo, Wilayani Rutshuru, mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa serikali katika jimbo la Kivu Kaskazini kutoka Wilaya ya Rutshukuru wamewashtumu waasi wa FDLR Rudi kwa kutekeleza mauaji hayo kwa kuwapiga risasi wanajeshi hao.

Elie Nzaani bunge wa eneo hilo anasema mbali na watu hao, wanajeshi wengien walitekwa katika kijiji cha Katwiguru na kuongeza kuwa, mauaji yameendelea kuzua hali ya wasiwasi.

Kwa upande wao watetezi wa haki za binadamu amewataka waasi wilayani Rutshuru pamoja viongozi wa serikali jimboni kivu Kaskazini kukaa kwenye meza moja kwa lengo la kudumisha amani na usalama wilayani humo.

Mwanaharakati Dunia Taabu amehuzunishwa kuona watu wanaendelea kuuawa wengi wakiwa ni raia wa kawaida.

Haya yanajiri wakati wananchi wamekuwa wakionyesha kuwa na imani na jeshi la nchi hiyo, huku wakiitaka serikali, kuongeza idadi ya askari wa kuulinda usalama wao kwenye maeneo yanayoshuhudia mapigano ya mara kwa mara

Hadi sasa ni zaidi ya raia kumi ndio wameripotiwa kuuliwa kikatili na waasi hao wanaodaiwa kuwa wa FDLR RUDI tangu mwanzo wa juma lililopita,lakini mpaka sasa hakuna kundi lolote lililo jitokeza kudai kuhusika na mauaji hayo.