MALI-USALAMA

Mali: Bamako yataka kuwasiliana na makundi mawili ya kigaidi

Iyad ag Ghali, kiongozi wa kundi la GSIM, wakati akipokelewa kwa mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Agosti 7 mwaka 2012.
Iyad ag Ghali, kiongozi wa kundi la GSIM, wakati akipokelewa kwa mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Agosti 7 mwaka 2012. AFP PHOTO / ROMARIC OLLO HIEN

Mwakilishi mkuu wa rais Ibrahim Boubacar Keïta katika eneo la Kati, Dioncounda Traoré, amebaini kwamba amewaagiza wajumbe wa serikali kuwasiliana na makundi mawili ya kigaidi.

Matangazo ya kibiashara

Habari hiyo imefichuliwa muda si mrefu, lakini inafahamika kwamba, miezi nne iliyopita, Dioncounda Traoré aliagiza maafisa kadhaa ambao walikuja kupendekezwa kuwa wasimamizi wa wa mazungumzo na makundi ya kigaidi yenye silaha.

Wiki chache zilizopita mwakilishi mkuu wa rais Keita aliamua, kuwafuta kazi wajumbe wapya. Amesema yuko tayari kuwaagiza wengine ikiwa itahitajika.

Mchakato huu ambao ulifichuliwa Alhamisi wiki hii, kwa kweli umethibitishwa na ofisi ya rais wa Mali.

Lengo ni kuanzisha mawasiliano ya moja kwa moja ili kuona kama mazungumzo yanawezekana, hasa na viongozi wawili: Iyad Ag Ghali na Amadou Koufa.

Dioncounda Traoré anamjua Iyad Ag Ghali, kutoka GSIM, kundi linalounga mkono Uislam na Waislam. Alikuwa katika serikali mwanzoni mwa miaka ya 1990, wakati Tuareg walipoanzisha uasi chini ya uongozi wa Iyad Ag Ghali. Hata hivyo, wawili hao hawajaonana kwa karibu muongo mmoja.

Kiongozi wa pili wa kundi la waasi ambaye Bamako inataka kufanya naye mazungumzo ni Amadou Koufa, kiongozi wa katiba ya Macina, kundi ambalo linaendelea kuhatarisha usalama katikati mwa Mali tangu mwaka wa 2015.

Kwa sasa, hakuna mawasiliano yoyote ambayo yamefanywa ili kukutana kwa mazungumzo na Abu Walid al-Sahraoui, mkuu wa kundi la Islamic State katika Grand Sahara.

Awali Dioncounda Traoré alikuwa kwenye ,stari wa kwanza kupinga mazungumzo yoyote na makundi ya kigaidi nchini Mali.

"Ikiwa leo tunaweza kuokoa hata kifo kimoja, lazima tujaribu mazungumzo," Dioncounda Traoré amebaini. Inabakia kuanzisha mawasiliano ya moja kwa moja. Ni hatua ya kwanza na sio rahisi. Iyad Ag Ghali na Amadou Koufa wanashuku mpango huo kwa sababu wanajua wanasakwa nchini Mali na wana hofu ya kukamatwa baada ya kuanzisha mpango huo wa mazungumzo.