Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-USALAMA

Watatu wauawa katika makabiliano na vikosi vya usalama Labe, Guinea

Mmoja wa waandamanaji akikabiliana na vikosi vya usalama, Oktoba 24 huko Conakry (picha ya kumbukumbu).
Mmoja wa waandamanaji akikabiliana na vikosi vya usalama, Oktoba 24 huko Conakry (picha ya kumbukumbu). CELLOU BINANI / AFP

Watu watatu wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama katika mji wa Labé, katikati mwa Guinea, Alhamisi wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Labé ni moja maeneo yanayopinga kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba iliyoombea na Rais wa nchi hiyo Alpha Condé.

Mamia ya waandamanaji waliingia mitaani mapema asubuhi lakini dadikika chache baadae kulizuka makabiliano kati ya waandamanaji hao na vikosi vya usalama ambavyo vilitumia risasi za moto kwa kuzima maandamano hayo.

Wakaazi wa mji wa Labé wameendelea kungiliwa na wasiwasi mkubwa baada ya hali kutokea Alhamisi wiki hii.

"Nimechukizwa na kile ambacho kimetokea hivi karibuni," afisa wa serikali ya mji wa Labé amesema.

Tangu mapema asubuhi mji wa Labé uko katika hali ya utulivu, lakini raia bado wanazungumzia hali iliyotokea jana Alhamisi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.