DRC: Watu wengi wauawa katika shambulio jipya Beni

Waasi wa Uganda wa ADF wanaendelea kuwalenga raia katika mashambulizi ya Mashariki mwa DRC.
Waasi wa Uganda wa ADF wanaendelea kuwalenga raia katika mashambulizi ya Mashariki mwa DRC. John WESSELS / AFP

Raia wanaendelea kulengwa katika mashambulizi lmbalimbali katika mji wa Beni na viunga vyake. Kulingana na ripoti ya awali kuhusu mauaji yaliyotokea usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, watu 38 waliuawa katika eneo hilo la mashariki mwa nchi.

Matangazo ya kibiashara

Wiki mbili kabla, jeshi la la DRC, FARDC, lilidhibiti eneo la Madina, ambalo ni ngome ya waasi.

Lewis Saliboko, mmoja wa wahariri wa mashirika ya kiraia katika mji wa Beni, amesema wahanga waliuawa kwa visu na pamoja na mapanga.

Watu wawili waliojeruhiwa vibaya wanaendelea kupata huduma za matibabu, kwa mujibu wa Lewis Saliboko, huku akiongeza kwamba hali kwa sasa ni ya kusikitisha.

"Jeshi kudhibiti haikuwakata tamaa waasi. Operesheni ya jeshi ilipelekea waasi hao kutawanyika" , amesema Lewis Saliboko.

Raia wanaendelea kulengwa katika mashambulizi yanayotekelezwa na makundi mbalimbali ya silaha Mashariki mwa DRC.