ZIMBABWE-UCHUMI

Serikali ya Zimbabwe na vyama vya wafanyakazi wafikia makubaliano

Mtumishi wa umma akiandamana na bango katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
Mtumishi wa umma akiandamana na bango katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare. AFP/Jekesai Nijikizana

Hatimaye serikali ya Zimbabwe na vyama vya wafanyakazi nchini humo wamekubaliana kuwaongezea mshahara wafanyakazi ambao wamekuwa wakigoma kwa kipindi kirefu sasa.

Matangazo ya kibiashara

Gazeti la serikali the Herald limeripoti kuwa makubaliano yamefanyika kati ya pande hizo mbili, baada ya mazungumzo ya muda mrefu.

Makubaliano hayo yanaeleza kuwa, mfanyakazi wa chini sasa atalipwa Dola 146 kila mwezi sawa na Dola za Zimbabwe 2,5000.

Vyama vya wafanyakazi nchinni humo licha ya kukubali nyongeza hii, vimesema kuwa, ni asilimia 31 ya nyongeza, kinyume na kile ambacho walikuwa wanakitafuta.

Mgomo wa Madaktari ulimalizika nchini humo mwezi huu baada ya tajiri Strive Masiyiwa, kujitolea kuwalipa Dola 300 kila mwezi, hadi miezi sita wakati serikali ya rais Emmerson Mnanagagwa ambayo inakabiliwa na chnagamoto kubwa ya kiuchumi, itakapopata suluhu ya suala hilo.