ZIMBABWE-UCHUMI-MGOMO

Bilionea Strive Masiyiwa akubali kulipa mishahara ya madaktari

Strive Masiyiwa Novemba 2015 huko New York.
Strive Masiyiwa Novemba 2015 huko New York. Jemal Countess/Getty Images International Rescue Committee/AFP

Raia raia wa Zimbabwe na mwanzilishi wa shirika la Telecom (Econet), ameahidi kufadhili sehemu ya mshahara wa madaktari katika hospitali za umma kwa miezi sita ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Madaktari hawa wamekuwa kwenye mgomo kwa zaidi ya miezi minne wakilaani mazingira ya kazi na hasa mishahara yao, ambayo imeporomoka kwa sababu ya mfumko wa bei nchini.

Shughuli zimezorota kwa miezi kadhaa katika hospitali za umma nchini Zimbabwe. Kunaripotiwa uhaba wa dawa, uhaba wa maji safi, Huku sehemu kubwa ya madaktari imeacha kufanya kazi. Mshahara wao wa kila mwezi - ambao ni chini ya dola 200 - umekuwa haukidhi mahitaji yao.

Strive Masiyiwa ameahidi kutoa dola za Marekani milioni sita ili kuwalipa madaktari 2,000, ambapo kila mmoja atalipwa mshahara wa dola 300 kwa mwezi, kwa kipindi cha miezi sita ijayo.

Madaktari wengi tayari wamekubali ombi hilo na wamekubali kurejea kazini, amesema Tawanda Zvakada, msemaji wa Chama cha Madaktari wa Hospitali za Umma.

Hayo yanajiri wakati serikali ya Zimbabwe na vyama vya wafanyakazi nchini humo walikubaliana wiki hii kuwaongezea mshahara wafanyakazi ambao wamekuwa wakigoma kwa kipindi kirefu sasa.

Makubaliano hayo yanaeleza kuwa, mfanyakazi wa chini sasa atalipwa Dola 146 kila mwezi sawa na Dola za Zimbabwe 2,5000.