DRC-AFYA-USALAMA

Maabara ya dawa inayochangia kupambana dhidi ya Ebola yateketea kwa moto Bukavu

Mji wa Bukavu, ambapo maabara ya dawa, mali ya Kanisa Katoliki, iliteketea kwa moto.
Mji wa Bukavu, ambapo maabara ya dawa, mali ya Kanisa Katoliki, iliteketea kwa moto. Wikimedia/EMMANRMS

Kanisa Katoliki la Bukavu, katika mkoa wa Kivu Kusini, Mashartiki mwa DRC, limepoteza maabara yake ya kutengeneza dawa, baada ya kuteketea kwa moto Jumatano wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Maabara hii ilikuwa mali ya ya ofisi ya Dayosisi ya kazi za matibabu (BDOM). Iliteketezwa na moto, ambao chanzo chake inaaminika kuwa ni kukatika ghaflya kwa umeme.

Maabara hii ilichangia kwa uzalishaji wa klorini ili kupambana na kuenea kwa virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola katika mkoa wa Kivu Kusini.

Askofu Mkuu wa Bukavu, François-Xavier Maroyi, amebaini kwamba sio waumini wa Kanisa Katoliki pekee ambao wameoteza bali ni wakaazi wote wa mkoa wa Kivu Kusini.

"Ninajua kuwa kuna watu wengi wamepigwa na butwaa baada ya kusikia tukio hili. Tumekua tukihudumia mkoa mzima, katika maeneo 34. Kwa mfano, tulikuwa tukitoa dawa mbalimbali na bidhaa zingine za kila aina. Inamaanisha kuwa gharama itakuwa kubwa mno. Naamini uongozi wa mkoa unajua hasara tuliyoipata, " amesema Askofu Mkuu wa Bukavu, François-Xavier Maroyi.

Mkurugenzi wa BDOM, Padri Paul Babikire, ukarabati wa maabara hiyo utagharimu dola milioni moja na nusu, na pia vifaa vinaweza kugharimu dola milioni moja.

Waziri wa Afya Cosmos Bishisha aambaye aliwasili katika eneo la tukio ameahidi kwamba serikali itachangia katika ukarabati wa jengo hilo.