Pata taarifa kuu
GUINEA-BISSAU-SIASA-USALAMA

Ushindi wa Umaro Sissoco Embalo wathibitishwa

Bango la kampeni la mgombea urais Umaro Sissoco Embalo, aliyeibuka mshindi wa uchaguzi wa urais Guinea-Bissau.
Bango la kampeni la mgombea urais Umaro Sissoco Embalo, aliyeibuka mshindi wa uchaguzi wa urais Guinea-Bissau. SEYLLOU / AFP

Hatimaye Mahakama kuu nchini Guinea Bissau imethibitisha Matokeo ya uchaguzi wa rais, yaliyotangazwa hivi karibuni na Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kuwa kiongozi wa upinzani Umaro Sissoco Embalo ndiye mshindi wa uchaguzi wa duru ya pili ya urais huku chama tawala cha PAIGC kikiyapinga matokeo.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya uchaguzi imethibitisha ushindi wa Umaro Sissoco Embalo katika uchaguzi wa urais, baada ya ya kurejelea kuhesabu kura za duru ya pili kama ilivyoombwa na Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ili kujaribu kuitoa nchi hiyo katika mvutano wa kisiasa.

Mwezi mmoja baada ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliyofanyika Desemba 29, mvutano unaendelea kujitokeza kati ya Umaro Sissoco Embalo, kutoka chama cha upinzaji, na Domingos Simoes Pereira, mgombea wa PAIGC, chama ambacho kimetawala Guinea-Bissau kwa miongo kadhaa.

Hata hivyo bado mvutano kati ya Tume ya uchaguzi na Mahakama Kuu ya nchi hiyo, unaendelea.

Hatua mpya imefikiwa katika mzozo wa Guinea-Bissau, lakini bado mivutano inaendelea. Baada ya mgombea aliyeshindwa kupinga matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais, na kukata rufaa katika Mahakama Kuu, Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) ilipendekeza, wiki iliyopita, kuchukuliwe hatua "ya kipekee".

Tume ya uchaguzi ilitakiwa kurejelea hesabu za kura za duru ya pili ya uchaguzi wa urais, jambo ambalo tume hiyo ilifanya na kuthibitisha kwamba Umaro Sissoco Embalo alishinda uchauguzi huo akiongoza kwa 53.55% ya kura dhidi ya 46.45% ya kura alizopata Domingos Simoes Pereira.

Mshindi aliyetangazwa, Umaro Sissoco Embalo, amekaribisha hatua hiyo, na mpinzani wake hajaamini mpaka sasa. Kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, PAIGC imelaanii, kwa mara nyingine tena, kile inachokiona kama ukosefu wa uwazi wa tume ya taifa ya uchaguzi, na kubaini kwamba itaendelea kukata rufaa mahakamani.

Katika mahojiano na kituo mama cha televisheni ya ufaransa France 24, juma moja lililopita Sissoco alisema kuwa alijuwa kuwa yeye ndiye rais mteule wa taifa hilo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.