Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Nigeria: Zaidi ya watu 30 waangamia katika shambulio la kijihadi

Jeshi la Nigeria likijiandaa kuzingira eneo ambapo mtu mmoja aliuawa na watu wasiojulikana katika shambulio dhidi ya Jimbo la Polo huko Maiduguri Februari 16, 2019.
Jeshi la Nigeria likijiandaa kuzingira eneo ambapo mtu mmoja aliuawa na watu wasiojulikana katika shambulio dhidi ya Jimbo la Polo huko Maiduguri Februari 16, 2019. REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Zaidi ya watu 30 waliuawa Jumapili usiku katika shambulio la wanamgambo wa Kiislamu karibu na kijiji jirani na mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri, eneo ambalo kundi la Islamic State Afrika Magharibi (ISWAP) ) linaendesha uhalifu wake, kulingana na vyanzo rasmi.

Matangazo ya kibiashara

Waasi "waliuwa zaidi ya watu 30, wengi mwa waliouawa walikuwa abiria ambao walikuwa wanasafiri kwenye barabara kati ya Maiduguri na Damaturu- na walichoma moto magari 18," msemaji wa serikali Ahmad Abdurrahman Bundi amesema katika taarifa, na kuongeza kuwa "wanawake na watoto wengi wametekwa nyara".

Mmoja wa wanamgambo wanaopigana dhidi ya wanajihadi kwa kulisaidia jeshi la serikali amebaini kwamba amehesabu malori 30 ambayo yaliteketea kwa moto.

"Madereva wengi wa malori na wasaidizi wao waliuawa, baada ya kuchomwa moto wakiwa hai kwa walipokuwa usingizini," Babakura Kolo ameliambia shirika la Habari la AFP.

Wapiganaji pia walizuia mabasi matatu yalikuwa yakielekea Maiduguri lakini ilibidi yasimame, kama magari mengine, kwa sababu ya jeshi ya kutotoka nje au kusafiri usiku.

"Haijulikani ni wanawake wangapi na watoto waliotekwa nyara, lakini idadi yao ni kubwa" ameongeza Babakura Kolo. Wanajihadi pia walipora katika kijiji jirani cha Auno, kilomita 25 kutoka Maiduguri, kabla ya kuchoma moto nyumba kadhaa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.