SUDAN-ICC

Sudan kumkabidhi Bashir katika mahakama ya ICC

Rais wa zamani wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir akiwa mahakamani mjini Khartoum, September 28, 2019.
Rais wa zamani wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir akiwa mahakamani mjini Khartoum, September 28, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah/File Photo

Mamlaka nchini Sudan imetangaza kuwa itamkabidhi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, rais wa zamani wan chi hiyo Omar al-Bashir.

Matangazo ya kibiashara

Bashir anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya halaiki, makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kutokana na kuhusika kwake katika machafuko ya jimbo la Darfur mwaka 2003.

Kiongozi huyo aliondolewa madarakani mwezi April mwaka jana kufuatia maandamano ya wananchi waliokuwa wakishinikiza aondoke madarakani.

Bashir aliingia madarakani madarakani mwaka 1989 kupitia mapinduzi ya kijeshi na kuiongoza nchi hiyo kwa mkono wa Chuma.

Waendesha mashtaka katika mahakama ya ICC kwa muda mrefu wamekuwa wakitaka Bashir aende kujibu mashtaka yanayomkabili kuhusiana na mauaji ya Darfur.

Kwa mujibu wa umoja wa mataifa, watu wanaokadiriwa kufikia laki 3 waliuawa na wengine Zaidi ya milioni 2 na laki 5 walipoteza makazi yao.

Mwezi Desemba mwaka jana, Bashir alihukumiwa kifungo cha miaka 2 kwenda katika kituo cha mafunzo ya watu waliohukumiwa kwa makosa ya rushwa.

Waendesha mashtaka nchini Sudan pia wamemfungulia mashtaka ya mauaji ya waandamanaji waliokuwa wakishinikiza aondoke madarakani.