SUDAN-ICC-BASHIR-HAKI

Serikali ya Sudan na waasi waafikiana kuhusu hatma ya washtakiwa wa ICC

Ingawa hajatajwa hata kwa jina na kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Khartoum katika mazungumzo na makundi ya waasi, rais wa zamani Omar al-Bashir anahusika na makubaliano yaliyopatikana Jumanne hii, Februari 11.
Ingawa hajatajwa hata kwa jina na kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Khartoum katika mazungumzo na makundi ya waasi, rais wa zamani Omar al-Bashir anahusika na makubaliano yaliyopatikana Jumanne hii, Februari 11. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir anaweza kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai siku za usoni.Tangazo hili lililotolewa Jumanne na kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Khartoum mwishoni mwa kikao kipya cha mazungumzo na makundi ya waasi.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo halimaanishi kwamba Omar al-Bashir anaweza kufikishwa mbele ya mahakama hiyo haraka iwezekanavyo.

"Tumefikia makubaliano kuhusu watu waliopatikana na hatia na ICC, nayasema haya waziwazi, " alisema Mohamed Hassan Altaishi, kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Khartoum katika mazungumzo na makundi ya waasi.

Wale waliohusika na "uhalifu dhidi ya binadamu" na "uhalifu wa kivita" uliofanywa Darfur wanaweza kukabidhiwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, " aliongeza Hassan Altaishi.

"Tumekubaliana leo kuhusu kufikishwa ICC kwa mtu yeyote ambaye anasakwa na mahakama hiyo" alibainia Bw Hassan Altaishi.

Kauli hii inaonyesha kuwa rais wa zamani Omar al-Bashir atahusika na uamuzi huu. Kwa sababu ikiwa hajatajwa jina na kiongozi huo wa ujumbe wa serikali katika mazungumzo na makundi ya waasi, yeye ni mmoja wa watuhumiwa na ICC.

Hii ni moja tu ya masuala ya makubaliano mapana yanayojadiliwa kwa sasa huko Juba na makundi ya waasi ya Darfur na sehemu zingine za Sudan.

Moja ya maswali ya kujadiliwa

Suala hili limetajwa kama moja wapo ya masuala ambayo yanapaswa kujadiliwa kati ya viongozi wa mpito wa Sudan na makundi ya waasi wanaokutana katika mazungumzo nchini Sudani Kusini kujadili amani ya kudumu.

Mamlaka ya Khartoum ilitoa ahadi hii wakati wa mazungumzo ya amani na makundi ya waasi ya Darfur. Makundi haya ya waasi yalikuwa yakidai kwamba rais wa zamani apelekwe ICC.

Suala hili limezua mvutano Khartoum, hasa kati ya taasisi kuu za uongozi wa nchi. Na hakuna makubaliano rasmi ambayo yametangazwa - hadi leo - wakati tarehe iliyoahidiwa ya kutia saini kwenye makubaliano hayo inakaribia.