Pata taarifa kuu
DRC-MAHAKIMU-MGOMO

Mgomo wa Mahakimu nchini DRC washika kasi

Rais wa DRC  Félix Tshisekedi
Rais wa DRC Félix Tshisekedi Sumy Sadurni / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Mgomo wa Mahakimu unaendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kudai nyongeza ya mshahara na kuboreshewa mazingira ya kufanya kazi.

Matangazo ya kibiashara

Hali hii inashuhudiwa licha ya hapo awali, kuwepo kwa  mazungmzo kati ya Mahakimu hao na Waziri wa sheria, bila mafanikio.

Watumishi hao muhimu wa idara ya Mahakama, wanataka ahadi ya nyongeza ya mshahara iliyolewa na rais wa zamani Joseph Kabila kutekelezwa, kabla ya wao kurudi kazi.

Mgomo huo wa nchi nzima, umesababisha kukwama kwa kesi mbalimbali katika Mahakama za nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

“Hii serikali haisemi lolote kuhusu suala hili, ndio maana tumeamua kugoma, na tutaendelea hivi labda kwa miezi kadhaa ili tujibiwe,” walisema Mahakimu wanaogoma.

Hatua hii imechelewesha na kusababisha kuahirishwa kwa kesi kadhaa, huku wafungwa wakiwa hawafahamu hatima yao kwa sababu, shughuli zinaweza kurejelewa tu baada ya mgomo huo kuisha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.