COTE D'IVOIRE-MAZUNGUMZO-SIASA

Serikali ya Cote d'Ivoire yasitisha mazungumzo ya kisiasa

Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire Amadou Gon Coulibaly Aprili 14 huko Abidjan.
Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire Amadou Gon Coulibaly Aprili 14 huko Abidjan. ISSOUF SANOGO / AFP

Baada ya mazungumzo ya mwezi mmoja na nusu, mazungumzo ya kisiasa kati ya serikali na upinzani yanaonekana yamekwama tena, miezi nane kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Jana, mkutano ambao ulitakiwa kumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo ulimalizika kwa kuhitimisha mazungumzo hayo, bila ya kutia saini kwenye makubaliano. Sasa rais Alassane Ouattara ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.

"Vyama vya siasa kutia saini katika mfumo wa mazungumzo ya kisiasa". Hii ni mada ya kikao cha Jumatatu jioni ambayo wengi wanasema ni mada albayo ilikuwa wazi ten amuhimu kwa nchi ya Cote d'Ivoire ambayo inajiandalia uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika ndani ya miezi nane ijayo.

Baada ya kuchelewa kwa saa moja kulingana na ratiba na dakika tano tu za hotuba iliyopongeza "maendeleo ya demokrasia", Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly alifunga kikao hicho, na kuamua kuhitimisha mazungumzo haya.

Upande wa upinzani, ambapo PDCI na muungano unaoongozwa na Dchama cha cha FPI Laurent Gbagbo vilivyowakilishwa katika mkutano huo, wamesema wameshangazwa na uamuzi huu.

Jean-Gervais Tchéidé, naibu kiongozi wa muungano unaosimamia uchaguzi, amebaini kwamba "Waziri Mkuu alihitimisha mazungumzo hayo wakati tulikuwa tumefikia kwenye hatau nzuri. Tulishangawa na uamuzi huo. "

Wakati serikali na upinzani walikuwa wameweza kukubaliana juu ya ulipaji wa gharama za kampeni kwa zaidi ya 5% ya kura, madai mengine, kama vile kuachana na mashtaka yanayomkabili Laurent Gbagbo nchini Cote d'Ivoire au uhuru zaidi kwa Tume ya Uchaguzi, yaliwekwa kando, upinzani umelalama.

Waziri Mkuu alisema kuwa "atatoa ripoti hizi kwa rais na kwamba rais mwenyewe atatoa maamuzi yake kuhusu masuala hayo". Kwa upande wao, vyama vya upinzaji vimebaini kwamba mkutano na waandishi wa habari utafanyika leo Jumanne katika makao makuu ya chama cha PDC.