SUDAN-ICC-BASHIR-HAKI

Kesi ya Omar al-Bashir ICC: Kauli ya viongozi wa Sudan yatia mashaka

Rais wa Sudan Omar al-Bashir afikishwa mahakamani Khartoum, Agosti 31, 2019.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir afikishwa mahakamani Khartoum, Agosti 31, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Wiki iliyopita, afisa mwandamizi wa Sudan alisema kwamba serikali ya Khartoum iko tayari kukabidhi Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Jinai (ICC) watu inaowashtumu makosa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na rais wa zamani wa Omar al-Bashir.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo mpaka sasa halijawekwa wazi na viongozi wa Sudan. Februari 17, waziri mmoja alitoa hoja zinazoangaliwa kutumiwa na mamlaka ya mpito ya Sudan.

Waziri wa Utamaduni na Habari na mwandishi wa zamani maarufu wa Sudan ambaye alizuiliwa jela chini ya utawala wa Omar al-Bashir, Faisal Saleh, ameelezea mipango ya mamlaka ya mpito ya Khartoum.

Ameliambia shirika la Habari la Reuters kwamba kuna mipango tofauti inayoangaliwa na mamlaka ya mpito nchini Sudan kuhusu watuhumiwa wa ICC. "Moja ya mipango hiyo ambayo inawezekana ni kwa maafisa wa ICC [Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu] kuja hapa na washtuhumiwa kufika mbele ya ICC hapa Khartoum," mji mkuu wa Sudan, " Faisal Saleh amesema.

"Au kutakuwa na mahakama ya mseto." Au labda washtumiwa "watahamishiwa Hague", makao makuu ya ICC, ameo,geza.

Mipango hii itajadiliwa katika mazungumzo kati ya mamlaka ya mpito ya Sudan na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), Waziri wa Utamaduni na Habari wa Sudan amebaini. Kufikia sasa, ICC haijatoa tamko juu ya suala hilo.

Hata hivyo Faisal Saleh amesema kwa vyovyote vile itatokana na mkataba utakaofikiwa kati ya Baraza Kuu kwa ajili ya Amani, taasisi inayojumuisha Braza Kuu tawala linalotawaliwa na wanajeshi, mawaziri (raia) na wawakilishi wa vyama vya siasa ambao walipinga utawala wa Omar el-Bashir.

Kwa upande wa watetezi wa haki za binadamu, wanasema habari njema ni Sudan kufanya juhudi za kufafanua msimamo wake.