ALGERIA-HAKI

Algeria: Mtoto wa rais wa Algeria kufungwa miaka miwili jela

Khaled Tebboune, mtoto wa rais wa Algeria, anashtumiwa kuwa na uhusiano na Kamel Chikhi anayehusishwa katika kesi ya biashara ya madawa ya kulevya.
Khaled Tebboune, mtoto wa rais wa Algeria, anashtumiwa kuwa na uhusiano na Kamel Chikhi anayehusishwa katika kesi ya biashara ya madawa ya kulevya. RYAD KRAMDI / AFP

Mwendesha mashtaka mkuu wa Jamhuri nchini Algeria ameomba kifungo cha miaka 10 jela dhidi ya Kamel Chikhi, mfanyabiasha mkubwa nchini humo, ambaye ni mtuhumiwa mkuu katika kesi ya "kufanya biashara kwa ushawishi" katika mali isiyohamishika.

Matangazo ya kibiashara

Pia Mwendesha mashitaka mkuu wa jamhuri ameomba kifungo cha miaka miwili jela dhii ya mtoto wa rais wa sasa wa Algeria Khaled Tebboune, anayehusishwa pia katika kesi hiyo.

Kesi ya Kamel Chikhi, mfanyabiashara aliyehusishwa katika kesi ya biashara ya madawa ya kulevya ilianza Jumatano wiki hii.

Wakati alipokuwa akisikilizwa mbele ya majaji, Kamel Chikhi alijaribu kumtetea mtoto wa rais, Khaled Tebboune, akihakikishia mahakama kuwa hajawahi kumsaidia kuhusiana na shughuli zake haramu za mali isiyohamishika.

Khaled Tebboune pia alikataa kuhusika kwake katika shughuli hiyo.

Khaled Tebboune anashtumiwa kuwa na uhusiano na Kamel Chikhi anayekabiliwa na mashitaka.

Lakini wakati wa uchunguzi, kufika kwa Khaled Tebboune katika ofisi za Kamel Chikhi kuliwashangaza wengi. Wachunguzi wanashuku kwamba mtoto wa rais Tebboune anahusika katika kesi nyingine inayohusu miradi ya mali isiyohamishika.

Hivi sasa akiwa kizuizini na washtakiwa wengine sita, Khaled Tebboune atakabiliwa na mashtaka kadhaa, pamoja na "kufanya biashara kwa ushawishi", "utumiaji mbaya wa madaraka", "ukusanyaji wa zawadi zisizofaa" na "ufisadi".

Aliwekwa kizuizini mnamo mwezi Juni 2018, mwaka na nusu kabla ya uchaguzi wa baba yake kama rais wa Algeria. Abelaziz Bouteflika wakati huo alikuwa bado rais.

Kamel Chikhi ndiye mtuhumiwa mkuu katika kesi ya hii ihusuyo kilo 700 za madawa ya kulevya aina ya Cocaine zilizokamatwa katika bandari ya Algeria mnamo mwezi Mei 2018.