UGANDA-TANZANIA-CORONAVIRUS

Uganda, Tanzania zatoa tahadhari kwa raia wake kuhusu virusi vya Corona

Pichani ni rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Pichani ni rais wa Uganda, Yoweri Museveni GAEL GRILHOT / AFP

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amewataka raia wa nchi hiyo kuacha kusabahiana kwa mikono kama tahadhari ili kuepusha kuambukizwa virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

 

Rais Museveni amesema “Sasa wakati Wizara ya afya inatuongoza, acheni tuchukue uamuzi wa kibinafsi kutoshikana mikono bila kujali au kujitokeza kwa hali ambazo zitarahisisha kuenea kwa Coronavirus”.

 

Hivi karibuni wizara ya afya iliwataka raia wake walioko nchini China kuterejea nyumbani hadi pale ugonjwa huo utakapodhibitiwa, akisema nchi yake haina uwezo wa kukabiliana nao.

 

Nchini Tanzania, waziri wa biashara, Innocent Bashungwa, amesema ufanyaji biashara na nchi ya China umeshuka kwa kiwango kikubwa tangu kuripotiwa kwa mlipuko wa ugonjwa wa viruso vya Corona nchini China.

 

Katika mahojiano yake na gazeti la The EastAfrican, waziri Bashungwa amesema tangu kuripotiwa kwa virusi hivyo, idadi ya abiria na bidhaa kutoka China imeshuka na kusababisha athari za kiuchumi.

 

Hali hii haishuhudiwi tu nchini Tanzania, mataifa mengine kama Kenya, Rwanda na Uganda nayo yameathirika pakubwa kutokana na wafanya biashara wengi kutegemea bidhaa za China.

 

Nchini Kenya na Rwanda hali ni kama hiyo ambapo viongozi wan chi hizo wamewataka wananchi kuchukua tahadhari ili kuepuka kupata maambukizi.

 

Wizara ya afya nchini Kenya juma hili ilijikuta katika shinikizo kubwa la kutakiwa kuwaeleza raia ni wapi raia waliotua na ndege kutoka China walipo, huku rais Kenyatta akiagiza kutengenezwa kwa kituo maalumu cha kuwatazama wagonjwa.