GUINEA-BISSAU-SIASA-USALAMA

Bissau: Serikali ya Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Sissoco Embalo yatawazwa

Licha ya wito wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), ambayo ilibaini kwamba haitatambua "taasisi itakayoundwa na kuwekwa kinyume na mfumo wa kikatiba na sheria", serikali ya Waziri Mkuu Nuno Gomès Nabiam, aliyeteuliwa na Umaro Sissoco Embalo, hatimaye imetawazwa.

Sherehe ya kutawazwa kwa serikali ya Waziri Mkuu Nuno Nabian (aliyeteuliwa na Umaro Sissoco Embalo) kwenye Ikulu ya rais jioni ya Jumatatu, Machi 2, 2020.
Sherehe ya kutawazwa kwa serikali ya Waziri Mkuu Nuno Nabian (aliyeteuliwa na Umaro Sissoco Embalo) kwenye Ikulu ya rais jioni ya Jumatatu, Machi 2, 2020. Charlotte Idrac / RFI
Matangazo ya kibiashara

Sherehe hiyo ilifanyika katika ikulu ya rais Jumatatu wiki hii, Machi 2, 2020.

Serikali hiyo inaundwa na mawaziri kumi na tisa, makatibu dola kumi na tatu, huku sherehe za kuapishwa kwa serikali hiyo zikihudhuriwa na maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi.

Waziri Mkuu mteule aliwasilisha vipaumbele vyake: usalama, elimu, huduma za kijamii, ingawa hakuna waziri waafya aliyeteuliwa.

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imetoa wito wa kukomesha "machafuko nchini" na imeshtumu vikosi vya ulinzi na usalama kuingilia masuala ya siasa nchini Guinea-Bissau.

Wakatri huo huo Mamadu Serifo Djaquité, aliyeteuliwa kuwa msemaji wa serikali, amepuuzia mbali madai hayo ya ECOWAS.

"ECOWAS inafanya yaliyo chini ya jukumu lake. Na sisi pia hapa tutajitolea kwa dhati kujadili na ECOWAS kwa njia iliyo wazi kabisa, " amsema Mamadu Serifo Djaquité.

Kwa sasa Guinea Bissau ina serikali mbili, licha ya taarifa ya ECOWAS, amabapo wengi wamehoji kuhusu msimamo jumuiya jiyo katika mzozo unaoendelea nchini.

Jumapili Machi , Spika wa Bunge la kitaifa, Cipriano Cassama, aliyetawazwa kama rais wa mpito siku ya Ijumaa jioni, alitangaza kwamba anajiuzulu wadhifa wake.

Katika taarifa fupi aliyoitoa akiwa nyumbani kwake huko Bissau, akilindwa na askari wa ECOMIB, kikosi cha askari wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi, ECOWAS, na baadhi ya askari wa Guinea, Cipriano Cassama alisema "usalama wangu uko hatarini". Amebaini kwamba Jumamosi jioni, kuna askari walikuja kuwatafuta walinzi wake. Amesema ana hofia usalama wake na wa familia yake.

Pia alisema anataka kuepusha "mapigano kwa maslahi ya taifa na raia wa Guinea-Bissau" na kulaani kitendo cha jeshi kushikilia kwa nguvu makao makuu ya Bunge la taifa.

Cipriano Cassama alitawazwa bungeni siku ya Ijumaa jioni na wabunge 52, hasa kutoka chama cha PAIGC. Kabla ya hotuba yake, Teodora Gomes, mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kihistoria, alimwomba asiachii ngazi na asitoe tangazo hilo la kujiuzulu, lakini ameamua kujiuzulu, mashahidi wamesema.