KENYA-SOMALIA-JUBALAND-USALAMA

Kenya yashutumu Somalia kuvamia ardhi yake

Rais wa Kenya Uhuru ameinyooshea kidole cha lawama Somalia akisema hatua ya wanajeshi wa Somalia kuingia Kenya ni kitendo cha uchokozi, na kubaini kwamba "Kenya hitoendelea kuvumilia hali hiyo."

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hapa ilikuwa Oktoba 30, 2017, aliitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama baada ya mapigano ya Jumatatu Machi 2, 2020.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hapa ilikuwa Oktoba 30, 2017, aliitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama baada ya mapigano ya Jumatatu Machi 2, 2020. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Jumatano wiki hii rais Kenyatta aliitisha kikao cha dharura cha baraza lake la usalama la kitaifa siku mbili baada ya mapigano Jumatatu Machi 2 kati ya jeshi la Somalia na lile la jimbo linalojitawa la Jubaland Mapigano hayo yalitokea karibu na mpaka na Kenya.

Serikali ya Kenya imemshtumu Mogadishu kwa kukiuka sheria uhuru wake na kuingia nchini humo.

Kulingana na Kenya, mapigano kati ya wanajeshi wa Somalia na wale wa Jubaland yalisababisha askari wa Somalia kuingia katika mji wa mpaka wa Kenya wa Mandera, ambapo "waliharibu mali za raia" na waliwatishia usalama wakazi wa mji huo, ” Kenya imesema katika taarifa, huku ikibaini kwamba "kitendo hicho cha uchokozi" haitoendelea kukifumbia macho.

Wabunge kutoka mji wa Mandera waliliambia shirika la Habari la AFP siku ya Jumatatu kwamba mashambulizi hayo yalikuwa mabaya hali iliyowafanya wakazi kuyatoroka makazi yao wakihofia usalama wao.

''Wacheni uchokozi wa mara kwa mara na badala yake angazieni mambo yenu ya ndani", amesema rais Kenyatta, huku akibaini kwamba "Kenya haitakubali kutumika kama sababu ya changamoto zinazoikumba Somalia kisiasa.

"Kenya imelazimika kuathirika pakubwa kutokana na hatua yake ya kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuweka amani na usalama katika nchi jirani ya Somalia" , ameongeza rais wa Kenya.

Mapigano hayo ya Somalia ni kisa cha hivi karibuni cha wasiwasi kati ya Mogadishu na serikali zake za kijimbo.

Mamlaka ya Jubaland mnamo mwezi Agosti iliishutumu Mogadishu kwa kuingilia uchaguzi wake na kutaka kumpindua madarakani rais wake Ahmed Madobe ili kuweza kujipatia uwezo wa kulidhibiti jimbo hilo.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne asubuhi wiki hii, Umoja wa Mataifa ulisema watu 56,000 walilazimika kuyatoroka makazi yao nchini Somalia kwa sababu ya mvutano katika Jimbo linalojitawala la Jubaland.