Uchaguzi wa urais Cote d'Ivoire: Alassane Ouattara hatowania tena urais
Imechapishwa:
Rais wa Coted'Ivoire Alassane Ouattara ametangaza Alhamisi, Machi 5, kwamba hatawania muhula mwingine katika uchaguzi wa urais uliyopangwa kufanyika Oktoba 2020.
Rais wa Coted'Ivoire ametoa kauli hiyo mbele ya wabunge waliokutana katika kikao cha Bunge.
"Mlinichagua kuongoza nchi yetu nzuri kwa mihula miwili, nimeendelea kuweka mbele umuhimu wa kutekeleza ahadi zangu. Kwa hali hiyo, nilipata nafasi nzuri wakati wa kupitishwa kwa Katiba ya Jamuhuri ya Tatu mwaka 2016, nikazungumza kwamba singependelea kuwania muhula mpya wa urais. Kwa hivyo, ningependa kutangaza kwa dhati kwamba nimeamua kutowania katika uchaguzi wa urais ujao, " rais wa Cote d'Ivoire amesema.
Tangazo hilo limewashangaza wengi ambao waliamini kwamba Bw Ouattara angeliwania kwa muhula mwingine.
Katika hotuba yake iliyodumu dakika arobani, Alassane Ouattara amelezea kwa kina kile alichokifanya kwa kipindi chote alihudumia nchi hiyo kati ya mwaka wa 2011 na 2020, akibaini kwamba hatua zimepigwa katika nyanja mbalimbali, hususan nyanja ya uchumi, kijamii, elimu na afya pia. Alassane Ouattara amesema anajivunia mchango aliotoa kwa taifa lake la Cote d'Ivoire.