TUNISIA-USALAMA

Vikosi vya usalama vyalengwa katika mashambulizi mawili mbele ya ubalozi wa Marekani Tunis

Sehemu inayozunguka ubalozi wa Marekani huko Tunis, baada ya shambulio lililolenga jengo hilo, Machi 6, 2020.
Sehemu inayozunguka ubalozi wa Marekani huko Tunis, baada ya shambulio lililolenga jengo hilo, Machi 6, 2020. RFI/François Picard

Afisa wa polisi ameuawa na wengine wanne, pamoja na raia mmoja, wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yaliyolenga vikosi vya serikali vinavyotoa ulinzi wa ubalozi wa Marekani jijini Tinis, nchini Tunisia.

Matangazo ya kibiashara

Hili ni tukio la kwanza la aina hiyo kutokea katika mji mkuu aw Tunisia, Tunis, kwa kipindi cha miezi minane.

Mwezi Juni 2019, mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS) huko Tunis yalionyesha jinsi gani makundi yenye msimamo mkali nchini humo yamejiimarisha, ingawa hali ya usalama imeimarika sana.

Mlipuko wa leo Ijumaa ulizua hofu katika maeneo ya Berges du Lac, karibu kilomita kumi kutoka katikati mwa mji mkuu, ambapo ubalozi wa Marekani unapatikana, na ambao unazungukwa na vizuizi vikubwa vya usalama.

"Ofisi yetu iko umbali wa mita 300 na eneo la mashambulizi, lakini mlipuko ulikuwa na nguvu kiasi kwamba madirisha ya jengo letu yalitikisika," Haykel Boukraa, 49, aliliambia shirika la Habari la AFP. "Hofu ilitanda kabisa. Marafiki zangu wameingiliwa na wasiwasi mkubwa (...). Hatuwa na imani kama kweli tungeondoka kwenda nyumbani au kusalia ofisini," Haykel Boukraa ameongeza.

Kikosi cha polisi kilipelekwa haraka kwenye eneo la tukio, huku kikisaidiwa na helikopta.