Mali: Iyad Ag Ghali akubali kushiriki mazungumzo na serikali
Imechapishwa:
Kundi linalodai kuunga Uislam na Waislam, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda- katika ukanda wa Maghreb linasema kiongozi wake yuko tayari kushiriki mazungumzo na serikali ya Mali, kulingana na taarifa iliyotolewa Jumapili Machi 8, 2020.
Kundi la GSIM, JNIM kulingana na ufafanuzi wake katika Kiarabu, ilimethibitisha kwamba halitoi sharti yoyote kwa kushiriki mazungmzo hayo, isipokuwa tu kuondolewa kwa vikosi vya Barkhane kutoka Ufaransa.
Nakala hiyo imetambuliwa na wataalam kadhaa katika masuala ya usalama katika ukanda huo na pia shirika la Habari la Mauritania, al-Akhbar.
Tunapaswa kumaliza "mzozo huu wa umwagaji damu" ambao umedumu kwa zaidi ya miaka saba, lakini kaabla ya kufikia hatua hiyo, kundikundi hilo linataka askari wa Ufaransa kuondoka katika ukanda huo.
Muungano huo wa kigaidi pia wito kwa serikali kuitaka Minusma, Tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kusitisha shughuli zake nchini humo.