FBI yashirikiana na maafisa wa Sudan kwenye uchunguzi kuhusu jaribio la mauaji lililomlenga Abdallah Hamdok

Vikosi vya usalama kwenye eneo la shambulio lililotibiliwa dhidi ya Waziri Mkuu Abdallah Hamdok, Machi 9, 2020.
Vikosi vya usalama kwenye eneo la shambulio lililotibiliwa dhidi ya Waziri Mkuu Abdallah Hamdok, Machi 9, 2020. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Maafisa wa upelelezi kutoka kikosi cha FBI cha Marekani wamewasili Khartoum kusaidia kuchunguza jaribio la mauaji dhidi ya Waziri mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari na utamaduni nchini humo Faisal Mohammed Saleh akithinitisha hilo amesema, ujio wa maafisa hao ni kuleta ujuzi wa hali ya juu katika kesi hiyo.

Jumatano wiki hii msemaji wa serikali ya Sudan alithibitisha kwamba timu ya FBI ilisawili jana asubuhi kushirikiana na maafisa wa uchunguzi wa Sudan.

Serikali imethibitisha tu kwamba watuhumiwa kadhaa wamekamatwa, ikiwa ni pamoja na raia wa kigeni, na kwamba mlipuko huo ulisababishwa na "kifaa cha kilichotengenezwa kienyeji kilichowekwa kando ya barabara".

Kwa mujibu wa Waziri wa Habari wa Sudan, timu ya FBI inaundwa na watu watatu.

Waziri mkuu Hamdok aliponea mauaji hayo siku ya Jumatatu baada ya msafara wake kushambuliwa.

Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambuli hilo, lakini siku moja baada ya shambulio hilo, serikali ilitangaza kwamba imechukua hatua kadhaa, hatua ambazo zimeelezwa kwamba zinawalenga wafuasi wa rais wa zamani wa Sudan Omar al Bashir.